HOME

Jan 10, 2012

RAIS JAKAYA KIKWETE AKUTANA NA UJUMBE KUTOKA GAMBIA IKULU!!

Rais Kikwete na Mh. Lamin Kaba
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete jioni ya leo, Jumatatu, Januari 9, 2012, amekutana na kufanya mazungumzo na mjumbe maalum wa Rais wa Gambia, Mheshimiwa Yahya A. Jammeh.


Katika mazungumzo hayo yaliyofanyika Ikulu, Dar es Salaam, mjumbe huyo maalum, Mheshimiwa Lamin Kaba ambaye pia ni Waziri wa Uvuvi, Maliasili na Masuala ya Bunge amemkabidhi Rais Kikwete ujumbe maalum kutoka kwa Rais Jammeh.


 Katika mazungumzo yao, Rais Kikwete na Mheshimiwa Kaba wamezungumzia masuala yanayohusu uhusiano kati ya Tanzania na Gambia na pia masuala ya Afrika na ya kimataifa.


 Mjumbe huyo maalum anatarajiwa kuondoka nchini kesho kwenda Nairobi, Kenya ambako anatarajiwa kukutana na viongozi wa nchi hiyo.


 Imetolewa na:


Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,


Ikulu,


DAR ES SALAAM.


09 Januari, 2012

No comments:

Post a Comment