Jean Ping |
Umoja wa Afrika (AU) leo umeongeza muda wa kuwa madarakani kwa mtendaji mkuu wa umoja huo Jean Ping baada ya uchaguzi ambao hakupatikana mshindi ambapo Nkosazana Dlamini-Zuma wa Afrika kusini alikuwa anawania nafasi hiyo.
Mwenyekiti wa sasa wa umoja huo rais wa Benin Thomas Boni Yayi amesema katika taarifa yake kuwa wameamua kumuongezea muda Ping mpaka mpaka mwezi June wakati wa kikao kingine kitakachofanyika Lilongwe nchini Malawi.
Ping raia wa Gabon ameiongoza tume hiyo tangu mwaka 2008, na alikuwa akiwania muhula mwingine lakini alishindwa kupata theluthi mbili zinazohitajika katika mpambano ambapo mke wa zamani wa rais wa Afrika Jacob Zuma, Dlamini-Zuma alikuwa anawania nafasi hiyo ambapo serikali ya Afrika kusini imesema Dlamini atawania tena nafasi hiyo.
No comments:
Post a Comment