HOME

Jan 30, 2012

WEZI WA MIFUGO WAUWA WATU 40 SUDAN YA KUSINI!!

Maeneo ya wafugaji Sudan



















Maafisa wa serikali katika Sudan Kusini wanasema takribani watu 40 wameuwawa na kundi la watu wenye silaha waliokwenda kuiba mifugo.

Baadhi ya taarifa zinasema idadi ya watu waliouwawa ni zaidi ya 100 kwenye uvamizi, huo uliotokea kwenye kambi moja katika jimbo la Warrap.

Waziri wa mambo ya ndani wa Sudan Kusini ameilaumu serikali ya Sudan kwa kuwapa silaha washambuliaji hao, ambao ni kundi la wapiganaji kutoka jimbo jirani la Unity.

Mvutano umeendelea kuwepo tangu Sudan Kusini ilipojitenga kutoka Sudan mwezi Julai, kufuatia vita vilivyochukua miaka mingi.

No comments:

Post a Comment