HOME

Jan 26, 2012

MADAKTARI WATAKIWA KUACHA MGOMO NA KURUDI KAZINI!!

Waziri wa afya na ustawi wa jamii wa Tanzania Dk. Hadi Mponda
























Wizara ya afya na ustawi wa jamii imewataka madaktari na watumishi wa afya wa umma ambao kwa sasa wapo katika mgomo usio na kikomo, kusitisha mgomo huo na kurejea katika vituo vyao vya kazi wakati serikali ikishughulikia madai yao.


Akizungumza jijini Dar es Salaam leo, waziri wa afya na ustawi wa jamii, Dk. Haji Mponda amewataka madaktari na watumishi hao wa afya kuandaa fursa ya kuwepo kwa mazungumzo na serikali kama alivyoagiza waziri mkuu jana wakati akingea na vyombo vya habari.


Kwa mujibu wa Dk. Mponda, madai ya watumishi hao ni ya msingi ingawa serikali imejitahidi kutatua baadhi ya madaio yao na kwamba kuna haja ya kukutana kumaliza tofauti zao kwa mazungumzo huku huduma za afya zikiendelea kama kawaida.

No comments:

Post a Comment