Rais Obama akizungumza wakati wa kikao kilichoandaliwa na kampuni ya huduma za tovuti ya Google. |
Rais Barrack Obama amekiri bayana kuwa jeshi la Marekani linatumia ndege za kivita zizizokuwa na rubani kulenga washukiwa wa wapiganaji wa kiislamu wa al Qaeda katika maeneo ya kiukoo nchini Paksitan.
Mashambulio ya kutumia ndege hizo za kivita yamekuwa mbinu kuu ya kupambana na wapiganaji wa al qaeda nchini afghanistan na Pakistan.
Kama sheria utawala wa rais obama haujadili mashambulio ya anga yanayotekelezwa na ndege za kivita zizizokuwa na rubani hadharani.
Na operesheni ya jeshi la marekani nchini Pakistan imekuwa jambo la siri.
No comments:
Post a Comment