Aisha Rashid 'Mwalala' katika harakati za kutafuta goli |
Etoo Mlanzi akisumbuana na mshambuliaji wa timu ya Namibia |
Poa Poa akionyesha makeke yake dimbani |
Timu ya taifa ya soka ya Wanawake 'Twiga Stars' jana ilianza vyema kampeni za kusaka tiketi za kufuzu kwa fainali za wanawake za Afrika baada ya kuifunga Namibia magoli 2-0 kwenye mchezo uliochezwa kwenye uwanja wa Sam Nujoma katika jiji la Windhoek nchini Namibia.
Timu hizo zilimaliza kipindi cha kwanza zikiwa hazijafungana.
Kipindi cha pili Twiga walitandaza soka safi na kupata mabao mawili kupitia kwa Aisha Rashid 'Mwalala' na Mwanahamisi Shuruwa.
Ushindi huo umeiweka Twiga Stars katika mazingira mazuri ya kufuzu hatua inayofuata kwa kuwa watakuwa na kazi rahisi kwenye mchezo wa marudiano utakaochezwa kwenye uwanja wa Taifa Januari 29.
Twiga ikifanikiwa kuwatoa Namibia watakutana na mshindi kati ya Misri na Zambia katika hatua nyingine.
Fainali hizo za Afrika kwa wanawake zitafanyia jijini Harare nchini Zimbabwe Novemba mwaka huu.
No comments:
Post a Comment