Mhe. Regia Mtema enzi za uhai wake. |
Gari aina ya Toyota Landcruiser VX (V8) likiwa limepata ajali na kusababisha kifo cha mbunge wa viti maalum kupitia Chadema Mh. Regia Mtema. |
Mbunge wa Viti Maalumu kupitia Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Regia Mtema amekufa katika ajali ya gari (pichani) iliyotokea jana saa tano na dakika kumi na tano asubuhi.
Mbunge huyo aliyekuwa akiendesha gari aina ya Toyota Landcruiser VX (V8) lenye namba za usajili T 296 BSM, alipasuka kichwa na ubongo wake kutapakaa katika eneo la ajali mita chache kabla ya kulifikia Daraja la Ruvu kutokea Dar es Salaam.
Mkuu wa Kikosi cha Usalama Barabarani mkoani Pwani, Kamishna Msaidizi wa Polisi (ACP), Saleh Mbaga amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo na kuongeza kuwa ilitokana na hatua ya Mbunge huyo kulipita gari lililokuwa mbele yake na ghafla likatokea roli la mafuta naalipotaka kurejea upande wake gari hilo lilimshinda na kupinduka na kubiringita mara saba.
Mbaga amesema baada ya kutokea kwa ajali hiyo, polisi walifika na kumkuta Mbunge huyo akiwa tayari amekufa huku akibubujikwa na damu nyingi kutokana na kichwa kupasuka huku ubongo ukiwa umemwagika ardhini.
Tunaipa pole familia,ndugu,jamaa na marafiki wa Mhe. Regia Mtema.
Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi Ameen!!
No comments:
Post a Comment