HOME

Jan 27, 2012

WAKENYA MILIONI TANO KUPATA VITAMBULISHO VYA UTAIFA KABLA UCHAGUZI MKUU UJAO!!

Waziri wa uhamiaji na usajili wa raia nchini Kenya Otieno Kajwang’
















Waziri katika baraza la mawaziri nchini Kenya amebainisha kuwa wananchi milioni tano wa Kenya watapata vitambulisho vya kitaifa kabla ya uchaguzi mkuu ujao wa nchi hiyo.


Waziri huyo wa uhamiaji na usajili wa raia Otieno Kajwang’ amesema Hazina ya nchi hiyo imetoa takribani shilingi bilioni 1.3 kwa ajili ya kufanikisha zoezi hilo.


Mr Kajwang’ amesema fedha hizo zitatumika kununulia rasilimali,kuajiri wafanyakazi zaidi na kufanya manunuzi ya magari mapya.

No comments:

Post a Comment