HOME

Jan 24, 2012

WABUNGE KUICHANGIA TWIGA STARS!!

Mechi ya Stars na Namibia iliyofanyika hivi karibuni




















Wabunge wa bunge la Tanzania watachangia kiasi cha fedha ambacho hakikutajwa kuisaidia timu ya taifa ya wanawake Twiga stars siku ya Alhamisi kuisaidia timu hiyo kuwa na maandalizi bora dhidi ya mchezo wao na Namibia.


Kulingana na afisa habari wa TFF Boniface Wambura,wabunge hao pia wanatarajia kuwa na mchezo wa kujiburudisha na timu hiyo mchezo utakaopigwa jioni ya Alhamisi kabla ya kutoa mchango wao.


Twiga stars itacheza na Nambia katika ninyanganyiro cha ubingwa wa Africa hatua ya awali mzunguko wa pili,mchezo utakaopigwa katika uwanja wa taifa jijini Dar es saaam siku ya jumapili.  

No comments:

Post a Comment