Rais Goodluck Jonathan akizungumza kwa njia ya Televisheni kuhusu kushusha bei ya mafuta ambayo ilisababisha migomo nchini Nigeria kwa takribani wiki nzima. |
Rais wa Nigeria Goodluck Jonathan leo ametangaza kushuka bei ya mafuta ya petrol kufuatia migomo na maandamano nchini humo ya kupinga ongezeko la bei ya mafuta.
Rais Jonathan amesema bei ya mafuta itashuka kwa asilimia 30 ikiwa ni kutambua hali ngumu ambayo wanainch wamekuwa wakiipitia.
Nchi hiyo ilikumbwa na migomo na maandamano na kusitisha shughuli mbali mbali za maendeleo baada ya serikali kutangaza kuondoa ruzuku ya mafuta kuanzia January mosi na kusababisha mafuta kuuzwa kwa naira 160 badala ya naira 40 kwa lita.
No comments:
Post a Comment