HOME

Jan 26, 2012

RAIS WA IOC ATARAJIA WANARIADHA KUTUMIA DAWA ZA KUONGEZA NGUVU MICHUANO YA OLIMPIC 2012!!

Rais wa IOC Jacques Rogge

Rais wa IOC Jacques Rogge amekiri kuwa anatarajia baadhi ya wanariadha watatumia dawa za kuongeza nguvu katika michuano ya Olimpiki itakayofanyika jijini London baadae mwaka huu.


Hatua kadhaa zimechukuliwa ikiwa ni pamoja na kuandaa maabara bora ikiwa ni pamoja na kuongeza asilimia kumi vifaa vya kufanyia uchunguzi ikilinganishwa na miaka minne iliyopita huko Beijing vitatumika kuwakamata wanamichezo watakaojaribu kudanganya.


Rogge amesema kila kitu ambacho kiko katika uwezo wa kibinadamu kimefanyika kwa ajili ya kupunguza nafasi ya matumizi wa dawa.

No comments:

Post a Comment