Mwakilishi wa Shirika hilo nchini Tanzania Bw. Oluseyi Bajulaiye |
Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuwahudumia Wakimbizi (UNHCR) linafanya mazungumzo na serikali ya Tanzania katika kufanikisha kuwarejesha nyumbani raia 200 wa Tanzania wanaoishi nchini Somalia.
Mwakilishi wa Shirika hilo nchini Tanzania Bw. Oluseyi Bajulaiye amesema serikali inataka kwanza kujiridhisha kwa kuwahakiki watanzania hao waliopo mjini Mogadishu, kabla ya kuridhia warejee nchini.
Bw. Bajulaiye amesema UNHCR inatarajia kuwarejesha nchini mwezi ujao raia hao wa Tanzania ambao wengi wao wanatokea visiwani Zanzibar na waliondoka nchini mnamo miaka ya 2001 na 2005.
No comments:
Post a Comment