Jan 29, 2012
MBUNGE ALIYEPATA AJALI NCHINI UGANDA BADO YUPO KWENYE HALI MBAYA!!
Mbunge wa bunge la Uganda Nabila Nagayi Ssempala bado yupo katika hali mbaya kufuatia ajali mbaya iliyotokea Ijumaa usiku iliyohusisha gari la lake na gari la doria la polisi.
Madaktari katika hospitali ya kimataifa ya Kampala (IHK) wanapanga kumfanyia uchunguzi zaidi wa kina kufahamu chanzo kamili cha maumivu yake makali.
Gari la mbunge huyo lilikumbana na gari la polisi katika barabara ya Namirembe karibu na nyumba ya watoto ya Sanyu Ijumaa usiku wakati akirejea kutoka kwenye mkutano wa hadhara wa kundi la Action for Change (A4C) katika uwanja wa Wankulukuku .
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment