HOME

Jan 26, 2012

MUUMINI AANGUKA NA KUFA KANISANI!!


Mshtuko uliwakumba waumini wa kikristo waliookoka wa kanisa la nguvu ya ukombozi lililopo mji wa Luweero nchini Uganda wakati mwanaume mmoja mwenye umri wa miaka 26 aliyekuwa akipokea
uponyaji kuanguka na kufa ndani ya kanisa hilo.


Mwanaume huyo Isaac Lubega mkazi wa kijiji cha Namukago jirani na wilaya ya Nakasongola alikufa majira ya saba usiku siku ya Jumatano wakati wa maombi ya asubuhi.


Chanzo cha kuanguka kulikopelekea kifo chake bado hakijafahamika lakini afisa wa polisi wilayani Luweero amesema polisi imeanza uchunguzi wa tukio hilo.


Siku chache kabla ya kifo chake mwanaume huyo alipelekwa kanisani hapo na mama yake ili apatiwe uponyaji kwa madai kuwa alikuwa na mapepo.

No comments:

Post a Comment