Jan 24, 2012
WAZIRI SITTA ATEMA CHECHE!!
Waziri wa Afrika Mashariki, mheshimiwa Samuel Sitta amesema haoni kama kuna mtu mwenye uwezo na mapenzi ya dhati ya kuiongoza Tanzania baina ya watu walio katika makundi yanayotajwa kuwania urais katika uchaguzi mkuu ujao.
Akizungumza jijini Dar es Salaam leo, mheshimiwa Sitta amesema wengi kati ya watu hao aidha hawana uwezo wa kuongoza nchi au wanakabiliwa na kashfa mbali mbali zinazowazuia kuwa viongozi wa jamii.
Ingawa ametetea kuwa si dhambi kwa mtu kutangaza nia ya kuwnia nafasi hiyo, mheshimiwa Sitta amesema kuna haja ya watu hao kupima sababu inayowasukuma kutaka kuingia ikulu kama ni ya dhati na yenye lengo la kutaka kuondoa maadui watatu wanaoikabili nchi ambao ni umaskini, ujinga na maradhi.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment