Majeruhi wa mashambulizi hayo akiwa amelazwa hospitalini Nigeria |
Kwa mujibu wa madaktari nchini Nigeria idadi ya vifo viliyotokana na shambulio la bomu siku ya ijumaa lililofanywa na kundi la kiislamu huko Nigeria inaongezeka.
Maafisa wa hospitali wanasema watu mia moja hamsini wamethibitishwa kuuawa lakini miili ya watu hao bado inaendelea kupelekwa katika chumba cha kuhifadhi maiti.
Boko Haram , wanaodai kuundwa kwa jimbo la kislamu wamesema sababu yao ya kufanya shambulio hilo ni kuwa vyombo vya kiusalama vimekataa kuwaachia huru wanachama wao waliokamatwa
Wakati huo huo katibu mkuu wa umoja wa mataifa Bw. Ban Ki-moon ameshtushwa na mashambulizi ya mabomu nchini Nigeria na kutaka ufanyike uchunguzi wa mamia ya vifo vilivyosababishwa na mashambulizi hayo.
No comments:
Post a Comment