HOME

Jan 19, 2012

RAIS KIKWETE AONGOZA MAMIA KATIKA MAZISHI YA REGIA MTEMA MJINI IFAKARA!!

Rais Kikwete (katikati) akiwa na viongozi wengine katika mazishi ya mbunge wa viti maalum Chadema Reagia Mtema yaliyofanyika Ifakara mkoani Morogoro.

Rais Kikwete akiweka udongo katika kaburi la Mh. Regia Mtema.




Rais Kikwete akiweka mashada ya maua katika kaburi la Mhe. Regia Mtema















































 Rais Jakaya Kikwete ameongoza maelfu ya wakazi wa Mji Mdogo wa Ifakara na waombolezaji wengine katika maziko ya Mbunge wa Viti maalum (CHADEMA) Regia Estelatus Mtema, yaliyofanyika katika makaburi ya Mkuliya,yaliyopo katika mji Mdogo wa Ifakara, wilayani Kilombero Mkoani Morogoro.


Mazishi ya Mbunge huyo aliyefariki dunia kwa ajali ya Gari iliyotokea Januari 14 mwaka huu eneo la Ruvu Mkoani Pwani, yametanguliwa na ibada na salamu za mwisho zilizotolewa na viongozi mbalimbali wa Serikali na chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) katika shughuli iliyofanyika kwenye Viwanja vya Kiungani,mjini humo.


Katika  Mazishi yaliyoingiliwa na mvua zilizoanza kunyesha saa chache kabla ya mazishi, baadhi ya wahudhuriaji wa mazishi hayo walizieleza kuwa ni baraka za kumsindikiza marehemu Regia kwenye nyumba ya mapumziko ya milele.


Mbali na Rais Kikwete, Mazishi hayo yamehudhuriwa na maelfu ya watu, wakiwemo viongozi mbalimbali ambapo mbali na Spika Makinda, walikuwepo pia Waziri wa Nchi Ofisi ya Raisi, Sera, Uratibu na Bunge Stephen Wasira na  Waziri waUtumishi Hawa Ghasia pamoja na wabunge kutoka vyama mbalimbali vya siasa wakati CHADEMA mbali na kuwakilishwa na wabunge wake wote, walikuwepo pia  Katibu Mkuu wa chama hicho Dk Wilbroad Slaa,
Mwenyekiti Mbowe na Naibu katibu mkuu wa chama hicho na mbunge wa Jimbo la Kigoma Kaskazini,Zito Kabwe.

No comments:

Post a Comment