Rais wa MAT Dk. Namala Mkopi |
Chama cha madaktari nchini Tanzania (MAT) kimetoa saa 72 kwa serikali kuhakikisha madaktari waliotimuliwa katika hospitali ya taifa Muhimbili wanarudishwa kazini.
Tamko hilo la MAT limetolewa na rais wa chama hicho Dk. Namala Mkopi katika mkutano wao na wanachama wote nchi nzima uliofanyika jijini Dar es salaam ambapo kimesema kinyume na matakwa yao kitaitisha mkutano mwingine mkubwa wa wanachama wote Jumatano ijayo kutoa uamuzi wao.
Aidha chama hicho kimemsimamisha uanachama Mganga mkuu wa serikali Dk. Deo Mtasiwa kwa muda wa mwaka mmoja kwa kosa la kusaliti fani ya udaktari Tanzania.
No comments:
Post a Comment