HOME

Jan 19, 2012

CTI YAGOMEA ONGEZEKO LA BEI YA UMEME!!


Shirikisho la wenye viwanda nchini Tanzania (CTI) limepinga hatua ya mamlaka ya udhibiti wa huduma za nishati na maji EWURA, ya kuongeza bei ya umeme kwa wastani wa asilimia 40.29.


Mwenyekiti wa CTI, Bw. Felix Mosha amesema hatua hiyo itaongeza gharama za uzalishaji viwandani na kufanya bidhaa za Tanzania kuwa ghali na kutohimili ushindani katika soko ndani na hata nje ya nchi.


Mh. Mosha amesema wao kama wazalishaji wanapendekeza ongezeko la kati ya asilimia ishirini na ishirini na tano, huku akiitaka Tanesco kupunguza kiwango cha umeme kinachopotea kabla ya kuwafikia wateja pamoja na kurekebisha viwango vya mishahara na matumizi ya ofisi ili viwe sawa na mashirika mengine duniani.

No comments:

Post a Comment