Klabu ya Yanga |
John Njoroge |
Mabingwa wa soka Tanzania bara timu ya Yanga ya jijini Dar es salaam imesema hijapokea barua kutoka shirikisho la soka duniani (FIFA) likiiagiza Yanga kumlipa mchezaji wake wa zamani raia wa Kenya mlinzi John Njoroge zaidi ya shilingi millioni 17 ikiwa ni fidia baada ya Yanga kusitisha mkataba ambao ulikuwa haijaisha.
Inasemekana FIFA iliiagiza Yanga kumlipa Njoroge kiasi hicho cha fedha baada ya mlinzi huyo kukata rufaa Fifa baada ya Yanga kushindwa kuahidi kulipa fedha hizo.
Katibu mkuu wa Yanga Mwesigwa Selestine amesema klabu hiyo haijapata barua kutoka Fifa na hivyo haiwezi kulishuhgulikia jambo hilo.
No comments:
Post a Comment