Jan 17, 2012
MAKAMU WA RAIS DK GHARIB BILAL LEO AMEWAONGOZA MAMIA YA WANANCHI KUUAGA MWILI WA MHE. REGIA MTEMA!!
Makamu wa Rais wa Tanzania Dk. Gharib Bilal leo amewaongoza mamia ya wananchi katika kutoa heshima za mwisho kwa aliyekuwa mbunge wa viti maalum (Chadema) Regia Mtema katika ukumbi wa Karimjee Jijini Dar es Salaam.
Zoezi hilo la kutoa heshima ya mwisho kwa marehemu Regia Mtema aliyefariki dunia jumamosi kwa ajali ya gari mkoani Kibaha wilayani Pwani, lilihudhuriwa pia na baadhi ya mawaziri, wabunge, wanasiasa pamoja na wananchi mbalimbali.
Shughuli hiyo inafuatiwa na mazishi yake yatakayofanyika kesho mjini Ifakara wilayani Kilombero mkoani Morogoro ambako Rais Jakaya Kikwete anatarajia kuongoza waombolezaji, katika kuupumzisha mwili wa marehemu Regia katika makazi yake ya milele.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment