HOME

Jan 13, 2012

NCCR MAGEUZI KUKATA RUFAA KUPINGA BEI MPYA YA UMEME!!

Naibu Katibu mkuu wa NCCR-Mageuzi, Bw. Faustine Sungura


Chama cha upinzani cha NCCR-Mageuzi cha nchini Tanzania, kimepanga kukata rufaa katika tume ya ushindani kupinga nyongeza ya bei ya umeme, kama ilivyotangazwa jana na mamlaka ya udhibiti wa huduma za nishati na maji (EWURA).


EWURA jana ilitangaza ongezeko la bei ya umeme kwa wastani wa asilimia 40.29, baada ya shirika la umeme nchini (TANESCO) kuomba nyongeza ya asilimia 155 kutokana na kile ilichodai kuwa ni kupanda kwa gharama za uendeshaji.


Lakini akizungumza jijini Dar es Salaam leo, Naibu Katibu mkuu wa NCCR-Mageuzi, Bw. Faustine Sungura amesema hatua ya wao kukata rufaa katika tume ya ushindani inatokana na ukweli kuwa ongezeko hilo litasababisha kupanda kwa mfumuko wa bei sambamba na kupanda kwa gharama za maisha, hali aliyodai kuwa itaathiri maisha ya Mtanzania wa kawaida.

No comments:

Post a Comment