Dkt Lucy Nkya |
Wizara ya afya na ustawi wa jamii nchini Tanzania, imewataka madaktari ambao kwa wiki kadhaa wmekuwa katika mvutano na serikali, kurejea katika vituo vyao vya kazi vinginevyo hatua za kinidhamu zitachukuliwa dhidi yao.
Msemaji wa wizara hiyo, Bw. Nsachris Mwamwaja amesema agizo hilo limetolewa na naibu waziri wa afya, Dkt Lucy Nkya kufuatia hatua ya mheshimiwa naibu waziri kutaka kukutana na madaktari hao kushindikana hapo jana.
Aidha, Mwamwaja amesema bado milango ya majadiliano ipo wazi katika kufikia muafaka wa madai yao na kwamba majadiliano yanaweza kuendelea huku madaktari wakiendelea na majukumu yao kwenye vituo vyao vya kazi ili kutoathiri utoaji wa huduma za afya.
No comments:
Post a Comment