Eneo la Mapwe Pande |
Serikali ya Tanzania imeanza zoezi la kuwahamisha wahanga wa mafuriko kutoka makamabini na kuwakabidhi viwanja eneo la mabwepanbe huku Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Said Meck Sadik akiishinikiza wizara ya maji kuharakisha uthibitisho wa maji ya visima vitatu kati ya sita vinavyotarajiwa kutoa huduma eneo hilo na kuepuka gharama kubwa za kusomba maji kwa kutumia magari.
Katika zoezi hilo lililoanza na kaya 289 pia Mkuu wa mkoa aliyetumia muda mwingi kukagua maendeleo ya huduma za maji,umeme na barabara ambapo mafundi wa shirika la umeme waliokuwa katika hatua za kutandaza nyaya walimthibitishia matarajio ya kuwasha umeme ndani ya wiki inayoanza huku mamlaka ya maji safi na maji taka Dar es salaam (DAWASA) ikileza kusubiria majibu ya sampuri kutoka maabara wizara licha kuwasilishwa zaidi ya wiki moja sasa
No comments:
Post a Comment