HOME

Jan 29, 2012

UHURU KENYATTA AGOMA KUJIUZURU KAMA NAIBU WAZIRI MKUU!!

Naibu waziri mkuu wa Kenya Uhuru Kenyatta

Naibu waziri mkuu wa Kenya Uhuru Kenyatta amesema hatojiuzuru wadhifa huo kufuatia mashtaka ya uhalifu dhidi ya binadamu yaliyothibitishwa na mahakama ya kimataifa ya makosa ya uhalifu (ICC).


Kenyatta amesema kamwe hataondoka katika kiti hicho licha ya mashinikizo kadhaa ya kumtaka aachie ngazi kama naibu waziri mkuu.


Pia ameendelea kusisitiza kubaki madaraka kama moja ya manaibu waziri wawili wa nchi hiyo na kuongeza kuwa kura ya kutokuwa na imani nae bungeni ndio pekee itakayomuondoa madarakani.

No comments:

Post a Comment