HOME

Jan 24, 2012

WANATAALUMA WA AFYA KUJIUNGA KATIKA MGOMO WA MADAKTARI!!

Hospitali ya taifa Muhimbili

Mgonjwa katika hospitali ya Muhimbili akielezea hali ilivyo baada ya madaktari na wanataaluma wa afya kutangaza kuanza mgomo.




















Huduma za afya katika zahanati na hospitali mbali mbali nchini zipo katika hatari ya kuzorota hasa baada ya wanataaluma ya afya kuungana na madaktari kutangaza mgomo wa nchi nzima usiokuwa na kikomo.


Mwenyekiti wa wanataaluma hao Dkt Stephen Ulimboka na mjumbe wa kamati ya wanataaluma, Dkt Edwin Chitage amesema kuwa hali katika mahospitali ni mbaya na kwamba hatua yao ya kugoma isitafsiriwe kwamba hawataki kuwatumikia Watanzania.


Mgomo huo umekuja baada ya wiki kadhaa za malumbano baina ya shirikisho la madaktari—MAT na wizara ya afya na ustawi wa jamii kuhusu maslahi na mazingira bora ya kufanyia kazi.


Wakifafanua namna wanavyoendesha mgomo wao, wamesema wameamua kuacha daktari mmoja tu katika kitengo cha mifupa cha hospitali ya taifa Muhimbili—MOI na kwamba hali katika hopsitali nyingine nchini ni mbaya.

No comments:

Post a Comment