Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe. Mizengo Pinda |
Chama cha wafanyakazi wa serikali kuu na afya hapa nchini(TUGHE) kimemuomba Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe. Mizengo Pinda kukutana tena na viongozi wa chama cha madaktari (MAT) na kusikiliza kero zao licha ya kumkwepa kiongozi mkuu huyo wa serikali siku ya Jumapili iliyopita
Wito huo umetolewa mjini Musoma na Katibu Mkuu wa TUGHE Taifa Ally Kiwenge baada ya viongozi wa chama hicho cha madaktari kushindwa kuonana na Waziri Mkuu ikiwa ni sehemu ya kutafuta suluhu ya sakata la mgomo wa madaktari.
Bw. Kiwenge amesema kuwa kimsingi ameshangazwa na hatua hiyo ya ujumbe wa MAT wa kushindwa kumuona Mizengo Pinda licha ya mawasiliano na taratibu zote za kumtaka waonane naye kukamilika na matokeo yake kutofika katika meza ya mazungumzo kwa hatua zaidi na kuongeza kuwa bila majadiliano kero zao hazitaweza kushughulikiwa.
Amesema Waziri Mkuu akiwa kama mwajiri anamshauri kukubali tena kuonana na ujumbe huo wa MAT katika meza ya mazungumzo ili waweze kusikiliza hoja za kila upande na kuzitafakari kwa pamoja kabla ya kufikia muafaka utakaoleta muafaka kati ya pande hizo mbili za mwajiri na mwajiriwa.
No comments:
Post a Comment