HOME

Jan 12, 2012

EWURA IMEPANDISHA BEI YA UMEME!!

Haruna Masebu

Mamlaka ya udhibiti wa huduma za nishati na maji nchini Tanzania (EWURA) imepandisha bei ya umeme kwa wastani wa shilingi 94 kwa uniti moja, sawa na ongezeko la wastani wa asilimia 40.29.


Mkurugenzi mkuu wa EWURA, Haruna Masebu amesema ongezeko hilo ni tofauti na maombi ya awali yaliyowasilishwa na Tanesco iliyoomba bei ya umeme ipande kwa asilimia 155.


Kufuatia ongezeko hilo, Mkurugenzi wa uchumi wa EWURA, Felix Ngalamgosi ametangaza bei mpya zitakazodumu kwa kipindi cha miezi sita ambapo hakutakuwa na ongezeko la bei kwa watumiaji wa chini ya uniti hamsini kwa mwezi.

No comments:

Post a Comment