HOME

Jan 25, 2012

RAIS OBAMA ASHAMBULIA TOFAUTI YA MAPATO!!

Rais wa Marekani Barack Obama























Rais wa Marekani Barack Obama ameshambulia tofauti kubwa ya kimapato katika hotuba yake ya tatu ya mustakabali wa taifa ikiwa ni agenda yake kuelekea uchaguzi mkuu nchini humo mwezi Novemba.


Katika hotuba hiyo rais Obama aliweka msisitizo wa umuhimu wa uchumi ambao unamhusisha kila mmoja katika hotuba hiyo aliyoitoa katika bunge la Cogress mapema leo asubuhi na kuonyeshwa moja kwa moja na Luninga.


Obama alirudia wito wake wa matajiri kulipa kodi zaidi hatua ambayo inapingwa vikali na Republicans, katika hotuba hiyo ambayo hutazwama na wamarekani wengi kwa umakini mkubwa kutaka kujua mwelekeo wa nchi yao kiuchumi,kijamii na kisiasa.

No comments:

Post a Comment