Waziri wa mambo ya ndani Tanzania, Mhe. Shamsi Vuai Nahodha |
Waziri wa mambo ya ndani nchini Tanzania, Mhe. Shamsi Vuai Nahodha ametangaza kuifanyia mabadiliko makubwa, idara ya uhamiaji, kufuatia kuongezeka kwa wimbi la wahamiaji haramu wanaodaiwa kuingia nchini kwa kushirikiana na watumishi wa idara hiyo wasio waaminifu.
Waziri Nahodha amesema hayo jijini Dar es Salaam leo wakati akipokea msaada wa magari kumi na moja pamoja na boti tatu za doria, kwa ajili ya kudhibiti wahamiaji haramu zilizotolewa na serikali ya Japan kupitia Idara ya kimataifa inayojishughulisha na wahamiaji (IOM).
Mh. Nahodha amesema zoezi hilo linalenga kuimarisha uadilifu na litahusisha watendaji na maofisa wa makao makuu ya idara hiyo, kabla ya kuhamia katika idara na vitengo vingine vilivyo chini ya wizara ya mabo ya ndani ya nchi.
No comments:
Post a Comment