Jan 24, 2012
WANNE WAFA KATIKA MAPIGANO MAPYA NCHINI LIBYA!!
Watu wanne wamekufa katika mapigano yaliyoibuka kati ya majeshi ya serikali ya Libya na wafuasi wa kiongozi wa zamani wa nchi hiyo kanali Muammar Gaddafi katika mji wa Bani Wali kusini Mashariki mwa Tripoli.
Mmoja wa wanajeshi wa baraza la serikali ya mpito (NTC) ameviambia vyombo vya habari kuwa Majeshi ya zamani ya kanali Gadaffi yanaushikilia mji huo hivi sasa.
Mapigano hayo yameibuka baada ya wanajeshi wa serikali ya mpito kuwakamata wafuasi wa kanali Gadaffi ambapo mji wa Bani Walid ulikuwa moja ya miji ya mwisho ya kanali Gadaffi kuingia katika mgogoro.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment