HOME

Jan 19, 2012

TUGHE YATANGAZA MGOGORO NA SERIKALI!!

Chama cha wafanyakazi wa serikali kuu na afya hapa nchini (TUGHE) kimetangaza mgogoro na serikali na kuahidi kuifikisha mahakamani baada ya kuwapunguzia kima cha mishahara baadhi ya watumishi walioko katika ajira ya utumishi wa umma hivyo kuvunja sheria na kanuni zinazoongoza sekta  hiyo ya umma.

Miongoni mwa wizara zinazokusudiwa kushitakiwa na TUGHE ni pamoja na ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa sanjari na Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma ambazo ama kwa makusidi au kutaka watumishi waichukie serikali yao,zimekiuka waraka na maagizo ya Katibu Mkuu Kiongozi.

Katibu Mkuu wa TUGHE hapa nchini Bw. Ally Kiwenge ametangaza mgogoro huo mjini Bukoba baada ya kupata taarifa za watumishi mbalimbali wa serikali mkoa wa Kagera wakiwemo maafisa tarafa kuwa wamepunguziwa kima cha mishahara yao kwa kigezo cha kutokuwa na elimu ya shahada ya kwanza ya chuo kikuu,jambo ambalo ni kinyume cha sheria.

No comments:

Post a Comment