HOME

Jan 23, 2012

MWANAUME AWACHOMA MOTO WATOTO WAKE!!

Mama wa watoto hao akiwa hospitalini kuwahudumia

Mwanaume mmoja mwenye umri wa miaka 27 wilayani Pallisa nchini Uganda amewekwa mahabusu kwa kosa la kuwachoma moto watoto wake watatu.


Kwa mujibu wa gazeti moja la nchi hiyo Mwanaume huyo Tom Oboi wa kijiji cha Akisim nje kidogo ya mji wa Gogonyo anadaiwa kuwafungia watoto wake hao watatu katika nyumba ya nyasi kabla ya kuiwasha moto uliosababisha kifo cha mtoto mmoja na wengine kujeruhiwa vibaya.


Akizungumza na waandishi wa habari hospitalini mama wa watoto hao Betty Epalitai mwenye miaka 25 amesema siku hiyo ya tukio mume wake alikwenda kunywa pombe na kurudi nyumbani saa nne kamili usiku akiwa mkorofi na mwenye hasira.


Imeripotiwa kuwa mwanaume huyo alimwambia mke wake ametimiza lengo lake kabla ya kujisalimisha mikononi mwa polisi katika kituo cha Gogoyo.

No comments:

Post a Comment