Katibu wa Itikadi na Uenezi Nape Nnnauye akizungumza na waandishi wa habari Zanzibar. |
Katibu wa Nec,Itikadi na uenezi Nape Nnauye (katikati)Katibu mkuu wa Nec Uchumi na Fedha Mwigulu Nchemba na kulia katibu wa Nec,Siasa na Ushirikiano wa Kimataifa,Januari Makamba. |
Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) imemteua mfanyabiashara maarufu Mohammed Raza kutoka Zanzibar kuwa mgombea wa Uwakilishi jimbo la Uzini.
Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye amesema kwamba kikao hicho kilichofanyika chini ya Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete kimempitisha Raza baada ya kuridhika na sifa zake.
Nape amesema, Kamati Kuu pia imemteua Makamu Mwenyekiti wa CCM (Zanzibar), Dk. Aman Karume kufungua kampeni za CCM za kuwania jimbo hilo ambazo zitafanyika Januari 28, mwaka huu katika Uwanja wa mpira wa Ghana.
Pia amesema wakati kampeni zitafunguliwa na Dk. Karume, ufungaji kampeni hizo utafanywa na Rais mstaafu Ali Hassan Mwinyi kwenye Uwanja wa mpira wa Tunduni.
Uchaguzi mdogo wa uwakilishi jimbo la Uzini unafanyika kufuatia kufariki dunia aliyekuwa mwakilishi wake kwa tiketi ya CCM, Mussa Hamis Silima aliyefariki kwa ajali ya gari, Septemba 23, mwaka jana.
No comments:
Post a Comment