Cheka akimwonyesha ubabe Nyirawira |
Bondia Karama Nyirawila wa Dar es Salaam, ambaye aliamua kulitema taji la dunia la WBO, ili acheze pambano lisilo la ubingwa dhidi ya Francis Cheka ‘SMG’ wa Morogoro, amejikuta akipoteza mchezo huo uliochezwa kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
Licha ya kupoteza pambano hilo, lakini mashabiki waliofika uwanjani hapo waliondoka wakiwa wamesuuzika vilivyo kutokana na ushindani na uwezo uliooneshwa na mabondia hao.
Baada ya majaji kutoa uamuzi wao, Karama ambaye alitwaa tuzo ya Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA) ya Bondia Bora wa Ngumi za Kulipwa kwa mwaka 2011, alisema ameridhika na matokeo.
Naye Cheka amesema anafurahi kupata ushindi huo kwa kuwa hajawaangusha mashabiki wa ngumi wa mkoa wa Morogoro ambao wamekuwa wakimpa sapoti kubwa ikiwemo kujitokeza kwa wingi katika kila pambano analilocheza.
No comments:
Post a Comment