HOME

Apr 7, 2012

KILICHOTOKEA KUSABABISHA KIFO CHA KANUMBA NA HALI ILIVYO MSIBANI HIVI SASA!!

Hatman Mbilinyi akizungumza na wanahabari kuelezea anachokijua kuhusiana na msiba wa Steven Kanumba
Kamati iliyoundwa usiku baada ya kutokea msiba ikipanga jinsi shughuli nzima ya msiba wa Steven Kanumba ambaye amefariki usiku wa kuamkia leo nyumbani kwake Sinza Vatican ambapo uchunguzi wa mazingira ya kifo chake bado unaendelea.
Jackline Wolper mwenye mtandio wa Njano pamoja na waigizaji wengine wakiwa nyumbani kwa Marehemu Kanumba.
KWA MUJIBU WA MDOGO WA MAREHEMU STEVE KANUMBA, AMESEMA WALIKUWA NYUMBANI MAJIRA YA SITA USIKU AKAMWAMBIA AJIANDAE WATOKE LAKINI KUNA MTU WANAMSUBIRI NDIPO AKAONA GARI YA ELIZABETH MICHAEL  MAARUFU KAMA LULU IKIJA NYUMBANI YEYE AKAINGIA CHUMBANI KUWASUBIRI BAADAE AKASIKIA KAMA KIUGOMVI NA SIMU IKITAJWA KAMA CHANZO MUDA MFUPI LULU AKATOKA ANAKIMBIA HUKU NA KULE NA KUMUITA YEYE  KUMUAMBIA KANUMBA KAANGUKA, YEYE ALIPOENDA AKAMKUTA KAANGUKA NDIO AKAENDA KUMUITA DAKTARI WA KANUMBA NA ALIPORUDI HAKUMKUTA LULU NA KANUMBA ANATOKA MAPOVU MDOMONI, LAKINI  HADI TUNAVYOONGEA LULU YUKO POLISI OSTERBAY KWA AJILI YA MAHOJIANO NA POLISI.


Picha yake ambayo alipenda kuitumia kwenye profile mbalimbali ikiwa imewejkwa sebuleni kwake.
Msongamano wa magari mapema asubuhi katika barabara ya Vatican City Sinza nyumbani kwake watu ni wengi mno.
Gari likiingiza maturubai nyumbani kwa Kanumba.

Johari akilia sana
Steve akiwa amechoka baada ya kulia sana.
Gari ya Kanumba ikitolewa nje ya nyumba yake ili shughuli za msiba ziendelee ikiwemo kupanga viti na maturubai
Miss Tanzania mwaka 2006 Wema Sepetu akiwa katika eneo la msiba leo asubuhi.
Mwigizaji wa Filamu Irene Paul akilia kwa uchungu baada ya kufika msibani akiwa haamini kilichotokea.



1 comment: