HOME

Jan 12, 2012

HALI TETE NCHINI NIGERIA 'AMRI YA KUTOTOKA NJE YATANGAZWA'!!






Vijana wakiwa mitaani kufanya migomo
Mamlaka nchini Nigeria zimetangaza saa 24 za kutotoka nje katika Jimbo la Niger baada ya kundi la vijana kuingia mijini na kuchoma moto majengo na magari.


Vurugu katika jimbo la Minna zimekuja katika siku ya tatu ya migomo kitaifa kupinga hatua ya serikali kuondoa ruzuku katika mafuta kusababisha kupanda maradufu kwa bei ya bidhaa hiyo.


Vyama vya wafanyabiashara vinavyowakilisha wafanyakazi wa vituo vya mafuta nchini Nigeria vimetishia kuungana katika mgomo huo kwa kufunga uzalishaji wa mafuta.


Nigeria ni mzalishaji mkubwa wa mafuta barani Afrika lakini inaingiza petroli.

No comments:

Post a Comment