HOME

Jan 18, 2012

KIKAO CHA BARAZA LA WAWAKILISHI KIMEANZA LEO MJINI ZANZIBAR!!



















Kikao cha baraza la wawakilishi kimeanza leo Kisiwani Zanzibar huku wajumbe wa baraza hilo wakiwa wameanza kujadili muswada wa maslahi ya mafao ya viongozi wa kisiasa huku wajumbe wengi wakiupinga  na wengine wakitaka uondolewe.


Muswada huo ambao ulikataliwa mwaka jana  uliwasilishwa na waziri wa nchi afisi ya rais na mwenyekiti wa baraza la Mapinduzi Dk. Mwinyihaji Makame ambaye amesema muswada huo umefanyiwa marekebisho mengi baada ya kuonekana kuwa na kasoro nyingi ikiwemo mabadiliko ya malipo ya kinua mgongo na posho za utumishi..


Nao baadhi ya wajumbe waliochangia wametaka bado ufanyiwe marekebisho na asilimia zilizowekwa ni kubwa na zipunguzwe huku baadhi ya wawakilishi walitaka muswada huo uondolewe kwa vile hali za wananchi bado ni za kimaskini.

No comments:

Post a Comment