HOME

Jan 30, 2012

SUDAN YA KUSINI YAACHA KUCHIMBA MAFUTA!!

Uchimbaji mafuta Sudan

Sudan Kusini imesema imesimamisha uchimbaji wa mafuta, na haitoanza tena hadi maswala yote yaliyobaki na jirani yake, Sudan Kaskazini, yanapatiwa ufumbuzi.


Mazungumzo baina ya nchi mbili hizo kuhusu swala la mafuta, yalivunjika Ijumaa.


Sudan Kusini inasafirisha mafuta kwa mabomba yanayopita Sudan Kaskazini, lakini nchi hizo hazijakubaliana juu ya ujira unaofaa kuiipwa Sudan Kaskazini.


Waziri wa Mafuta wa Sudan Kusini, Stephen Dhieu Dau, amesema Sudan Kaskazini lazima iondoke katika jimbo la mzozo la Abyei, na iache kuwasaidia kifedha wapiganaji.

No comments:

Post a Comment