HOME

Jan 31, 2012

MAAFA MUHIMBILI!!

Wauguzi wakiwa nje ya hospitali Muhimbili



Siku moja tu baada ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda kuwataka madaktari kusitisha mgomo na kurejea kazini vinginevyo watajifukuzishwa kazi, hali imezidi kuwa mbaya katika hospitali ya Taifa Muhimbili na jana viliripotiwa vifo 10.


Mbali na hali ya vifo hivyo, madaktari wachache tu ndio walioripoti kazini jana, huku wengi wao wakiendelea na mgomo na wengine wakiishia kusaini kitabu cha mahudhurio kazini bila kuhudumia wagonjwa.


Mwenyekiti Chama cha Wauguzi Muhimbili (Tanna), Paul Magesa, akizungumza na waandishi wa habari jana alisema wamseshuhudia maiti 10 ndani ya wodi mbalimbali ambazo hazijathitishwa vifo na madaktari hadi ilipotimia jana mchana.


Wakati hali ikiwa hivyo, wauguzi nao jana waliungana na madaktari kugoma kufanya kazi wakitaka Pinda afute kauli yake ya kutaka kuwafukuza madaktari, ambao wangeendelea na mgomo jana.

No comments:

Post a Comment