HOME

Jan 29, 2012

JUMUIYA YA KIARABU IMESIMAMISHA SHUGHULI ZAKE NCHINI SYRIA!!

Wananchi wa Syria wakiwa katika migomo

Jumuia ya Nchi za Kiarabu imesimamisha shughuli za ujumbe wake wa uchunguzi nchini Syria.


Kiongozi wa jumuia hiyo, Nabil el Arabi, amesema uamuzi huo ulichukuliwa kwa sababu ya hali kuzidi kuwa mbaya nchini humo, huku ghasia zikiongezeka.


Jumuia hiyo iliongeza muda wa safari ya ujumbe wake baada ya mwezi wa kwanza kumalizika, lakini nchi za Ghuba ziliondoa wachunguzi wao, na hivo kupunguza hadhi ya ujumbe huo.

No comments:

Post a Comment