Jan 17, 2012
TANZANIA YATAKIWA KUTOSAINI MAKUBALIANO YA KIUCHUMI NA JUMUIYA YA ULAYA!!
Kikundi cha mazungumzo cha umoja wa makanisa nchini Tanzania (TEDG) kimeitaka serikali ya Tanzania na nchi za Afrika Mashariki kutosaini mkataba wa makubaliano ya kiuchumi na jumuiya ya Ulaya.
Mjumbe wa bodi ya TEDG, Nikibuka Shimwela amesema makubaliano yoyote na jumuiya ya Ulaya hayatakuwa na faida kwa Mtanzania wa kawaida kutokana na kile alichodai kuwa mijadala juu ya mikataba hiyo haipo wazi na ina harufu ya kinyonyaji.
Ameitaka serikali kuandaa mkakati wa kuwepo kwa uwakilishi mpana wa wananchi katika majadiliano hayo pamoja na kuelimisha umma juu ya ubia huo wa kiuchumi
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment