Mwenyekiti wa TAHLISO Paul Makonda |
Muungano wa wanafunzi wa ellimu ya vyuo vikuu Tanzania (TAHLISO) umesema hatua iliyochukuliwa na uongozi wa chuo kikuu cha Dar es salaam,Muhimbili na CBE Campus ya Dar es salaam kuwafukuza wanafunzi wa vyuo hivyo wakati wakidai haki ya wenzao ni unyanyasaji na ukandamizaji wa hali ya juu katika sekta ya elimu ya juu.
Hayo yamebainishwa na mwenyekiti wa TAHLISO Bw. Paul Makonda wakati akizungumza na waandishi wa habari Mjini Moshi kuhusiana na sakata la kufukuzwa kwa wananfunzi wa vyuo vikuu vya Dar es salaam wakiwemo viongozi wao.
Amesema uongozi wa vyuo hivyo haukutakiwa kuwafukuza wanafunzi hao bali kukaa na kutafuta chanzo na suluhu stahiki ya migomo na migogoro katika vyuo hivyo
badala ya kuhangaika na matokeo ya matatizo ambayo ni madai ya msingi katika vyuo.
No comments:
Post a Comment