HOME

Jan 23, 2012

BREAKING NEWS....ICC YATHIBITISHA MASHTAKA YA WATUHUMIWA WANNE KATI YA SITA WA VURUGU ZA UCHAGUZI KENYA!!

Jaji Ekaterina Trendafilovaakisoma uamuzi huo wa majaji wa mahakama ya ICC


























Majaji wa mahakama ya kimataifa ya makosa ya uhalifu (ICC) leo wamethibitisha mashtaka ya washukiwa wanne kati ya watuhumiwa sita wa vurugu za uchaguzi mkuu nchini Kenya waliotajwa na mwendesha mashtaka mkuu wa mahakama hiyo Bw. Luis Moreano Ocampo iwapo wana kesi ya kujibu ama laa.


Katika uamuzi huo ambao jaji Ekaterina Trendafilova anasoma hivi sasa moja kwa moja kutoka ICC majaji wa mahakama hiyo wamethibitisha kuwa mauaji yalifanyika katika uchaguzi huo ambapo waliothibitishwa kuhusika na vurugu hizo ni naibu waziri mkuu Uhuru Kenyatta,Mbunge wa Eldoret Kaskazini William Ruto,mkuu wa utumishi wa umma Francis Muthaura na mtangazaji wa kituo cha radio Joshua arap Sang,ambapo ,aliyekuwa waziri Henry Kosgey,alikuwa mkuu wa polisi Hussein Ali wametajwa kutohusika na vurugu hizo.
 

No comments:

Post a Comment