HOME

Jan 23, 2012

SERIKALI YAAGIZA WALIMU WAPYA WALIOAJIRIWA KARIBUNI WAPELEKWE VIJIJINI!!


Serikali ya Tanzania imewaagiza Wakurugenzi watendaji wa halmashauri zote nchini pamoja na maafisa elimu kusimamia zoezi la kugawanya walimu wapya walioajiriwa hivi karibuni ili kukabiliana na upungufu wa walimu hasa katika shule za vijijini.


Agizo hilo limetolewa na Naibu waziri ofisi ya waziri mkuu tawala za mikoa na serikali za mitaa elimu Mh. Kassim Majaliwa alipokuwa akifunga mafunzo  ya walimu wakuu wa shule za sekondari wa mikoa ya kanda ya nyanda za juu kusini yaliyofanyika mjini njombe.


Mh. Majaliwa amesema idadi hiyo ya waalimu wapya 23,219 inajumuisha walimu wa shule za msingi 10,648, walimu wa sekondari wenye shahada 6,674 na stashahada 5,897 ambapo amesema walimu hao wataanza kuripoti kuanzia tarehe 1 Mwezi ujao katika halmashauri walizopangiwa.

No comments:

Post a Comment