Rais Abdoulaye Wade |
Mahakama Kuu ya Senegal imetupilia mbali kesi ya rufaa ya vyama vya upinzani na kuthibitisha kuwa Rais Abdoulaye Wade anaweza kugombea kiti cha urais wa nchi hiyo kwa mara ya tatu.
Upinzani umesema katiba ya nchi hiyo imeweka kikomo cha mihula miwili, lakini mahakama hiyo imesema Bw. Wade hafungwi na sheria hiyo kwa sababu, sheria hiyo ilipitishwa akiwa katika muhula wake wa kwanza.
No comments:
Post a Comment