HOME

Jan 31, 2012

NYOKA WANAOZALIANA KWA KASI WAACHIWA NA KUANZA KULA WANYAMA!!



Kwa zaidi ya karne moja imekuwa ikisemekana kwamba nyoka wakubwa aina ya
Python wamesambaa katika sehemu iitwayo Everglades, kusini mwa jimbo la Florida.


Hata hivyo leo nyoka hao wamekuwa kitu halisi na wamesambaa sehemu kubwa ya eneo hilo.Nyoka wanaojulikana kama Burmese Pythons, ambao ni kati ya nyoka wakubwa zaidi duniani wamekuwa wakizaliana kwa kasi mno na kusambaa eneo hilo kiasi cha kutishia idadi ya wanyama wanaoishi huko.


Tayari zaidi ya nyoka 1000 wameshaondolewa kutoka Everglades tangu mwaka 2002, lakini idadi hiyo ni sehemu ndogo tu ya idadi halisi ya nyoka waliozagaa eneo hilo.


Kuwepo kwa nyoka hao katika eneo hilo kwa sehemu kumechangiwa na kuachiwa na watu waliokuwa wakiwafuga, ambao wameshindwa kuendelea kukaa nao kwa sababu ya kukua mno.Hali hiyo inaweza kuwa na madhara kwa maisha ya viumbe
wa eneo hilo kwa kuwa nyoka hao hula ndege na wanyama wa aina mbalimbali, wakiwemo jamii ya mamba.


Kutokana na kula kwao viumbe wa asili pamoja na kushindana na wanyama wawindaji wa eneo hilo, nyoka hawa wanaweza kuharibu utaratibu wa asili wa ikolojia ya Everglades.Hamu yao kubwa ya kula inaweza kuhatarisha zaidi wanyama walio katika hatari ya kutoweka ambao binadamu wanajaribu sana kuwa tunza.


Jitihada zinaendelea kujifunza zaidi namna ya kudhibiti idadi ya nyoka hao na kuzuia wengine wasiingie katika eneo hilio.

No comments:

Post a Comment