HOME

Jan 20, 2012

ICC KUAMUA HATMA YA WATUHUMIWA SITA WA KENYA!!



















 Mahakama ya kimataifa ya makosa ya uhalifu (ICC) leo imetoa taarifa kuwa majaji waliosikiliza shauri la awali la ikiwa watuhumiwa sita wa Kenya wana kesi ya kujibu au laa watatoa uamuzi huo siku ya Jumatatu wiki ijayo tarehe 23 Januari saa saba na nusu muda wa Kenya.


Taarifa hiyo ya kimahakama iliyotolewa leo kupitia akaunti ya twitter ya mahakama hiyo imesema majaji watatoa uamuzi huo katika chumba cha mahakama namba moja huko the Hague.


Watuhumiwa sita wa machafuko mara baada ya uchaguzi nchini Kenya ni naibu waziri mkuu Uhuru Kenyatta, mkuu wa utumishi wa umma Francis Muthaura na mbunge wa Eldoret Kaskazini Bw. William Ruto wengine ni mbunge wa Tinderet Henry Kosgey, mtangazaji wa radio Joshua arap Sang mkuu wa zamani wa jeshi la polisi Hussein Ali.

No comments:

Post a Comment