HOME

Jan 19, 2012

RIPOTI YA AJALI YA MV SPICE ISLANDES YATOLEWA!!

Meli ya spice islandes iliyozama mwezi Septemba mwaka jana eneo la Nungwi


Baadhi ya watu waliokuwa wakijaribu kujiokoa baada ya meli ya spice islandes kuzama

Serikali ya mapinduzi Zanziabr leo imeiweka hadharani ripoti ya tume ya rais iliyochunguza kuzama kwa meli ya spice islandes ambapo imetaka  watendaji wa serikali na wamiliki wa  meli akiwemo mjumbe wa baraza la wawakilishi wa Muyuni ambaye pia ni  mbunge wa kuteuliwa Mhe. Jaku Hashim Ayub washaitakiwe  kwa kusababisha ajali ya kuzama kwa meli hiyo na vifo vya watu zaidi ya 1500.


Akitangaza ripoti hiyo kwa waandishi wa habari Katibu mkuu kiongozi wa SMZ Bw. Abdulhamid Yahya Mzee amesema tume imependekeza watendaji wa bandari akiwemo mkurugenzi wa mamalaka ya baharini Bw. Haji Uusi na watendaji kadhaa washitakuwe kwa kusababishaa ajali hiyo ,huku pia ikipendeekza Mkurugenzi mkuu wa shirika la bandari Bw. Mustafa Aboud Jumbe naye achukuliwe hatua za kiniadhamu.....


Tune hiyo pia imethinbitiha kuwa meli hiyo iliyozama mwezi Septemba mwaka jana ilikuwa imebeba abiria 2470 badala ya 620 na idadi kubwa ya mzigo ambao uzito wake haujajulikana hali inayoonyesha kuwa watu 1326 wamepotea baharini na kufariki.


Kwa upande mwingine tume hiyo imependekeza fidia ya shilingi milioni 10 kwa kila aliyefariki na shiulingi milioni milioni 7 na nusu kwa waliosalimika lakini wameathirika na kupata ulemavu na shilingi milioni tano kwa waliosalimika.


Habari za kuaminika zaidi zilizopatikana ni kwamba tayari watendaji hao wa serikali watano akiwemo mkurugenzi wa mamlaka ya baharini Bw. Haji Uusi wamekamatwa na polisi na kuhojiwa na wako nje kwa dhamana.

No comments:

Post a Comment