HOME

Jan 18, 2012

WAKIMBIZI WAOMBA KUTAFUTIWA MASOKO!!

Mkuu wa mkoa wa Tanga Luteni mstaafu Chiku Gallawa

Serikali mkoani Tanga imewaagiza maafisa ushirika na biashara kuwatafutia masoko wakulima wa mahindi kufuatia wakimbizi wenye asili ya kisomali wanaohifadhiwa kisheria katika kambi ya Chogo iliyopo wilayani Handeni kulalamikia baadhi ya walanguzi kutoka nchi jirani ya Kenya kwenda kuwarubuni na kuwauzia kwa bei ya hasara kwa sababu ya kukosa soko.


Agizo hilo limetolewa na mkuu wa mkoa wa Tanga Luteni mstaafu Chiku Gallawa wakati alipotembelea kambi hiyo kisha kukagua ghala la mahindi ambayo yamekosa soko nchini.


Akizungungumza na wakimbizi hao mkuu huyo wa mkoa amesema maafisa hao wameajiriwa na serikali kwa ajili ya kuwasaidia wakulima ikiwemo kuwatafutia masoko na serikali itawapatia kibali cha kusafirisha hata nje ya nchi nia ikiwa ni kumsaidia mkulima aweze kunufaika na kilimo.


Awali akisoma risala kwa mkuu wa mkoa wa kiongozi wa wakulima wa wakimbizi hao Bw. Hassan Bashir amesema wamekuwa wakilima mazao tofauti lakini mahindi ni zaidi lakini wamekosa soko hatua ambayo imesababisha wafanyabiashara kutoka nchi jirani ya Kenya kwenda kuwarubuni wakulima kuwauzia kwa bei ya kutupa ili waweze kujipatian fedha ya kujikimu.


Hata hivyo pamoja na changamoto kwa wakimbizi hao mkuu wa mkoa amewataka kuwa makini katika kukabiliana na wimbi la wahamiaji haramu wa kisomali wanaoingia nchini mara kwa sababu wapo baadhi yao wanaweza kuwaficha katika kambi hiyo na kuhatarisha amani katika maeneo yao.

No comments:

Post a Comment